Bwana Yesu Atuliza Dhoruba

22 Siku moja Yesu alipanda mashua na wanafunzi wake akawaam bia, “Twendeni ng’ambo ya pili ya ziwa.” Kwa hiyo wakaanza kuvuka. Walipokuwa wakivuka, akalala usingizi. Upepo mkali ukawa unavuma na mashua yao ikaanza kujaa maji; wakawa katika hatari ya kuzama.

24 Wale wanafunzi wakamkimbilia Yesu wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana, tunazama!” Ndipo akaamka akaukemea ule upepo na yale mawimbi vikakoma, pakawa shwari.

Read full chapter