23 Kwa hiyo jihadharini kwa maana nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea.”

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

24 “Siku hizo, baada ya hiyo dhiki, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake. 25 Nyota zitaanguka kutoka mbinguni na nguvu za anga zitatikisika.

Read full chapter