Yuda Anapanga Kumsaliti Yesu

10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu kuwaambia kuwa yuko tayari kuwasaidia wamkamate Yesu. 11 Walifurahishwa sana na habari hizi, wakaahidi kumlipa fedha. Kwa hiyo yeye akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti.

Yesu Anakula Pasaka Na Wanafunzi Wake

12 Siku ya kwanza ya sherehe ya Mikate isiyotiwa chachu siku ambayo kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza Yesu, “Unapenda tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”

Read full chapter