17 Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 18 Walipokuwa mezani wakila, akawaambia, “Ninawaam bia hakika, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.” 19 Wote wakasikitika. Wakamwuliza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?”

Read full chapter