21 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama maandiko yasemavyo. Lakini ole wake yeye atakayenisaliti. Ingelikuwa heri kama hakuz aliwa!”

Chakula Cha Bwana

22 Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru , akaumega akawapa wanafunzi wake akisema, “Pokeeni, huu ni mwili wangu.” 23 Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa, wote wakanywa humo.

Read full chapter