Font Size
Marko 14:22-24
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Marko 14:22-24
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Chakula cha Bwana
(Mt 26:26-30; Lk 22:15-20; 1 Kor 11:23-25)
22 Na walipokuwa wakila Yesu aliuchukua mkate, akamshukuru Mungu kwa huo. Akamega vipande, akawapa wanafunzi wake, na kusema, “Chukueni na mle mkate huu. Ni mwili wangu.”
23 Kisha akakichukua kikombe chenye divai, akamshukuru Mungu kwa hicho, akawapa. Wote wakanywa toka kile kikombe. 24 Kisha akasema, “Kinywaji hiki ni damu yangu ambayo kwayo Mungu anafanya agano na watu wake. Damu yangu inamwagika kwa manufaa ya watu wengi.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International