29 Lakini nikisha fufuka nitawatangulia kwenda Galilaya. 30 Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.” Yesu akamwambia, “Ninakwambia hakika, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakanusha mara tatu kwamba hunifahamu.” 31 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama ni lazima niuawe pamoja nawe, sitakukana.” Na wale wanafunzi wen gine wote wakasema hivyo hivyo.

Read full chapter