35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa chi ni akaomba kuwa kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso aiepuke. 36 Akasema, “Aba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Tafadhali niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.” 37 Akarudi, akakuta wame lala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Hukuweza kukesha hata kwa saa moja?

Read full chapter