Add parallel Print Page Options

42 Amkeni! Twendeni! Tazama! Yule atakayenisaliti amekaribia.”

Yesu Akamatwa

(Mt 26:47-56; Lk 22:47-53; Yh 18:3-12)

43 Mara moja, wakati Yesu akali akizungumza, Yuda, mmoja wa wale kumi na mbili, alitokea. Pamoja naye walikuwa kundi kubwa la watu waliokuwa na majambia na marungu wakitoka kwa viongozi wa makuhani, walimu wa sheria na wazee.

44 Msaliti alikuwa tayari amewapa ishara: “Yule ambaye nitambusu ndiye mwenyewe. Mkamateni, mlindeni na muwe waangalifu mnapomwondoa.”

Read full chapter