54 Petro aliwafuata kwa mbali, akaingia barazani kwa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto. 55 Makuhani wakuu na wajumbe wote wa Baraza walijaribu kutafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo, lakini ushahidi wao haukupatana.

Read full chapter