Maskini mnao wakati wote na mnaweza kuwapa tia msaada wakati wo wote mtakapo. Lakini hamtakuwa nami wakati wote. Huyu mama amenitendea lile aliloweza. Amenipaka manukato kuniandaa kwa mazishi yangu. Nawaambieni hakika, mahali po pote duniani ambapo Habari Njema itahubiriwa, jambo hili alilo nitendea huyu mama, litatajwa kwa ukumbusho wake.”

Read full chapter