70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 71 Petro akaanza kulaani na kuapa, akawaambia, “Simjui huyo mtu mnayemsema.”

72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji Yesu

Read full chapter