14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”

15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.

Maaskari Wamdhihaki Yesu

16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari.

Read full chapter