15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.

Maaskari Wamdhihaki Yesu

16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika.

Read full chapter