Add parallel Print Page Options

17 Wakamvalisha Yesu joho la zambarau na wakafuma taji ya miiba na kumvisha kichwani. 18 Kisha wakaanza kumpigia saluti wakisema: “Heshima kwa Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga tena na tena kichwani kwa fimbo na wakamtemea mate. Kisha wakapiga magoti mbele yake na kujifanya wanampa heshima kama mfalme.

Read full chapter