Add parallel Print Page Options

Wafuasi wa Yesu ni Familia Yake Halisi

(Mt 12:46-50; Lk 8:19-21)

31 Kisha mama yake Yesu na nduguze wakaja. Wao walisimama nje na wakamtuma mtu aende kumwita ndani. 32 Humo lilikuwepo kundi lililoketi kumzunguka, lakini wao wakamwambia, “Tazama! Mama yako, kaka zako na dada zako wako[a] nje wanakusubiri.”

33 Yesu akauliza, “Mama yangu ni nani na kaka zangu ni akina nani?”

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:32 na dada zako wako Nakala zingine za Kiyunani hazina maneno haya.