Yesu Afafanua Maana Ya Mfano Wa Mbegu

13 Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Mtaelewaje basi mifano mingine? 14 Yule mtu aliyepanda mbegu, alipanda neno la Mungu. 15 Mbegu zilizoanguka njiani ni sawa na watu ambao husikia neno la Mungu na shetani akaja mara moja na kulichukua lile neno lililopandwa ndani yao.

Read full chapter