Add parallel Print Page Options

19 lakini mahangaiko ya maisha haya ya sasa, kuvutiwa na mali, na tamaa mbalimbali zingine huja na kulibana sana lile neno, nalo haliwezi kuwa na matokeo mazuri.[a]

20 Wengine ni kama mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri. Hawa ni wale wanaolisikia neno, na kulipokea na hivyo kuwa na matokeo mazuri; wengine kutoa thelathini, wengine sitini na wengine mia moja zaidi.”

Zingatieni Nuru

(Lk 8:16-18)

21 Yesu akawaambia, “Unapoileta taa ndani[b] je unaiweka chini ya bakuli ama uvungu wa kitanda? Au unaileta ndani na kuiweka juu ya kitako cha taa?

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:19 haliwezi kuwa na matokeo mazuri Kwa maana ya kawaida, “inakuwa haina matunda”, kwa maana kwamba watu hawa hawafanyi yale mambo mazuri ambayo Mungu anataka watu wafanye.
  2. 4:21 taa ndani Yesu anafananisha mafundisho yake kama taa iliyoletwa chumbani penye giza.