24 Akaendelea kuwaambia, “Myaweke maanani haya mnayosikia. Kipimo mnachotumia kwa wengine ndicho kitakachotumiwa kuwapima na ninyi, hata na zaidi. 25 Kwa maana aliye na kitu ataongezewa, na asiye na kitu atanyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”

Mfano Wa Jinsi Mbegu Inavyoota

26 Akawaambia tena, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.

Read full chapter