32 Hapo, watu walimletea kiziwi mmoja ambaye pia alikuwa hawezi kusema sawa sawa, wakamwomba amwekee mikono ili apone. 33 Yesu akampeleka yule kiziwi kando mbali na watu, akain giza vidole masikioni mwake kisha akatema mate na akaugusa ulimi wake. 34 Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akahema kwa uchungu, akamwambia, “Efatha!” yaani “Funguka!”

Read full chapter