34 Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akahema kwa uchungu, akamwambia, “Efatha!” yaani “Funguka!” 35 Wakati huo huo masikio ya yule mtu yakafunguka na ulimi wake ukawa huru akaanza kusema vizuri.

36 Yesu akawaamuru wasimwambie mtu ye yote habari hizi. Lakini kadiri alivyowazuia ndivyo walivyozidi kutangaza habari zake.

Read full chapter