34 Ndipo akawaita wale watu pamoja na wanafunzi wake aka waambia, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwe nyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 35 Kwa maana mtu ye yote aipotezaye nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, ataiokoa. 36 Mtu atafaidi nini kama atapata ulimwengu wote lakini akayaangamiza maisha yake?

Read full chapter