20 Wakamleta. Yule pepo alipomwona Yesu, alimtia yule mvulana kifafa, akaanguka chini akajiviringisha viringisha huku akitokwa na povu mdomoni. 21 Yesu akamwuliza baba yake, “Mwanao amekuwa na hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake. 22 Na mara nyingi huyo pepo amemwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kuangamiza maisha yake. Lakini kama wewe unaweza kufanya cho chote, tafadhali tuonee huruma, utusaidie.”

Read full chapter