24 Ndipo yule baba akasema kwa sauti, “Ninaamini. Nisaidie niweze kuamini zaidi!” 25 Naye Yesu ali poona umati wa watu unazidi kusongana kuja hapo walipokuwa, akam kemea yule pepo mchafu akisema, “Wewe pepo bubu na kiziwi, naku amuru umtoke, usimwingie tena!” 26 Yule pepo akapiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu kisha akatoka. Yule mvulana alionekana kama amekufa; kwa hiyo watu wengi wakasema, “Amekufa.”

Read full chapter