43 Kama mkono wako ukikusababisha utende dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili ukaingia katika moto usiozimika. [ 44 Huko funza hawafi wala moto hauzimiki.] 45 Na kama mguu wako ukikusababisha utende dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kiwete kuliko kuwa na miguu miwili ukaingia katika moto usiozimika. [

Read full chapter