Petro akamwambia Yesu , “Mwalimu, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Tutengeneze vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Musa na kingine cha Eliya.” Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.

Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, na sauti kutoka katika wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu nimpendaye, msikilizeni yeye.”

Read full chapter