17 Basi, kulikuwepo vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka wakati wa mfalme Daudi; na vizazi kumi na vinne tangu mfalme Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babiloni na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho hadi Kristo.

Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo

18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Mar ia akiwa bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri.

Read full chapter