14 Na kama mtu ye yote akikataa kuwapokea au kusiki liza maneno yenu, mtakapoondoka katika nyumba hiyo au mji huo, kung’uteni mavumbi yatakayokuwa miguuni mwenu. 15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”

Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso

16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.

Read full chapter