15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”

Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso

16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao.

Read full chapter