Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso

16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa.

Read full chapter