18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa. 19 Lakini mtakapokamatwa, msihangaike mkifiki ria mtakalosema; kwa maana mtaambiwa la kusema wakati huo. 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkizungumza bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akisema kupitia kwenu.

Read full chapter