39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

Read full chapter