24 Alipoanza kukagua hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa na deni la mamilioni ya shilingi, aliletwa kwake. 25 Na kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake aliamuru kwamba auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vyote alivyo navyo, ili zipatikane fedha za kulipa deni lake.

26 “Yule mtumishi akapiga magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’

Read full chapter