25 Na kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake aliamuru kwamba auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vyote alivyo navyo, ili zipatikane fedha za kulipa deni lake.

26 “Yule mtumishi akapiga magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 27 Yule bwana akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwachilia.

Read full chapter