34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia kweli, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” 35 Lakini Petro akasema, “Hata kama itabidi nife pamoja na wewe, sitakukana.” Na wana funzi wote wakasema hivyo hivyo.

Gethsemane

36 Kisha Yesu akaenda nao mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane. Akawaambia, “Kaeni hapa, mimi ninakwenda mbele zaidi kuomba.”

Read full chapter