69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui usemalo.”

71 Kisha alipotoka nje, mlangoni mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwapo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.”

Read full chapter