10 wakanunulia shamba la mfinyanzi kama Bwana alivyon iagiza.”

Yesu Mbele Ya Pilato

11 Yesu akapelekwa mbele ya gavana naye akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Hayo umetamka wewe.” 12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipomshtaki kwa mambo mengi hakujibu neno.

Read full chapter