Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” Kwa hiyo baada ya kujadiliana waliamua kuzitumia kununua shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. Kwa hiyo shamba hili limeitwa ‘Shamba la damu’ hadi leo.

Read full chapter