12 Pepeto lake liko mkononi, naye atasafisha pa kupepetea nafaka, na ngano yake ataiweka ghalani; lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”

Yesu Abatizwa

13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yordani ili abatizwe na Yohana. 14 Yohana alitaka kumzuia akimwambia, “Mimi ndiye ninahitaji kubatizwa na wewe, mbona unakuja kwangu? ”

Read full chapter