“Tubuni, muache dhambi zenu, mumgeukie Mungu; kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.” Huyu ndiye aliyezungumzwa na nabii Isaya aliposema, “Sauti ya mtu anayeita kwa sauti kubwa huko nyikani, ‘Tayarisheni njia ya Bwana, nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”

Yohana Mbatizaji alivaa nguo zilizotengenezwa kwa manyoya ya ngamia na kiunoni mwake alijifunga mkanda wa ngozi; chakula chake kilikuwa nzige na asali mwitu.

Read full chapter