Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Yudea yote na bonde lote la mto Yordani. Nao walipoungama dhambi zao aliwabatiza katika mto Yordani. Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili awabatize, aliwaambia, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya muepuke ghadhabu inayokuja?

Read full chapter