Wala msidhani mnaweza kujitetea mkisema, ‘Sisi ni wana wa Ibrahimu 10 Na hata sasa shoka la hukumu ya Mungu limewekwa tayari katika mashina ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa katwa na kutupwa motoni.

11 “Mimi nawabatiza kwa maji kama ishara kwamba mmetubu dhambi zenu. Lakini baada yangu anakuja aliye mkuu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuchukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Read full chapter