22 Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena.

23 “Basi, kama ulikuwa tayari kutoa sadaka yako madhaba huni, ukakumbuka kuwa ndugu yako amekukasirikia, 24 acha sadaka yako hapo hapo, uende kwanza ukapatane naye, kisha urudi kumtolea Mungu sadaka yako.

Read full chapter