Mafundisho Kuhusu Kuapa

33 “Tena mmesikia watu wa kale waliambiwa kwamba, ‘Usi vunje kiapo chako bali umtimizie Mungu kama ulivyoapa kutenda.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu.

Read full chapter