39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia; 40 na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili.

Read full chapter