44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo.

Read full chapter