ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Mafundisho Kuhusu Sala

“Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.

Read full chapter