Yesu Amponya Mwenye Ukoma

Alipotoka mlimani, umati mkubwa wa watu walimfuata. Na mtu mmoja mwenye ukoma akaja akapiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukipenda, unaweza kunitakasa.” Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Napenda. Takasika.” Wakati huo huo yule mtu akapona ukoma wake.

Read full chapter