Na mtu mmoja mwenye ukoma akaja akapiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukipenda, unaweza kunitakasa.” Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Napenda. Takasika.” Wakati huo huo yule mtu akapona ukoma wake. Na Yesu akamwambia, “Usiseme cho chote kwa mtu ye yote, lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani na utoe sadaka aliyoamuru Musa, iwe uthibitisho kwa watu kwamba umepona.”

Read full chapter