34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.”

Wafanyakazi Ni Wachache

35 Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu. 36 Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanateseka pasipo msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.

Read full chapter